Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe Gulam Hafeez akikagua
vifaa vya watoto wenye ulemavu wa Ngozi, Wasioona na kusikia baada ya
kukabidhiwa na Meneja wa NIC tawi la Shinyanga Bi Halima Makange.
Meneja wa NIC Tawi la Shinyanga Bi Halima Makange akitoa
vifaa vya huoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi,
wasioona na kusikia cha Buhangija Shinyanga, anayepokea msaada huo ni Msimamizi
wa kituo hicho Mwl Peter Ajali.
Meneja Wa NIC Tawi la Shinyanga Bi Halima Makange
akimuonesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe Gulam Hafeez vifaa vya watoto
wenye ulemavu wa Ngozi, wasioona na kusikia katikati ni Mlezi wa Kituo hicho Mwl
Peter Ajali Akishuhudia .
Mtaalamu wa Macho Fani ya Uoni hafifu kutoka Hospital ya
Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr. Ntoke Sospeter Wilson akiwaelezea watoto hao
namna ya kutumia darubini Kiona Mbali.
Meneja wa NIC Tawi la Shinyanga akiwa katikati ya watoto
wenye ulemavu wa Ngozi wa ngozi, wasioona na kusikia wakiwa wakijaribu kutumia kifaa cha Darubini Kiona Mbali katika kituo hicho Mjini Shinyanga.
No comments:
Post a Comment