Monday, May 25, 2015

UCHAGUZI MKUU WA SERIKALI 2015


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote  itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian  Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa  Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na  kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka – Oktoba 24 mwaka huu.
Halikadhalika siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.


Himahima mwananchi/mfanyakazi tujiandikishe katika daftari la kuduma la wapiga kura ili tusikose nafasi hii muhimu katika jamii na Taifa kwa ujumla. Kauli mbiu ya NIC kwa mwaka 2015 ni "Mfanyakazi jiandikishe, Kura yako inathamani kwa maendeleo yetu".

Friday, May 22, 2015

ZIARA YA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI TAWI LA SINGIDA

Msafara unaingia Tawi la Singida kwa ajili ya kikao na wafanyakazi 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sama kamanga akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi bima za maisha na Pensheni Bi. Rose Lutu Lawa

Maafisa bima wakifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi wa Bima za Maisha na Pensheni.



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji akifurahia jambo wakati kikao na wafanyakazi wa NIC tawi la Singida kikiendelea.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga akizungumza na mteja ambaye al;ikuwa akitoa malamiko kuhusu huduma za Bima.




Kaimu Mkurugenzi Mtendaji akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Bima tawi la Singida.

ZIARA YA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI TAWI LA DODOMA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga akiwa katika tawi la Dodoma tayari kwa kikao na maafisa bima wa tawi hilo.

Kaimu Mhasibu Mkuu Bi. Tabu S. Kingu akiwa katika ukumbi wa tawi la Dodoma tayari kwa kikao.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji akizungumza na maafisa bima tawi la Dodoma, kulia ni Mkurugenzi wa Bima za Maisha na Pensheni Bi. Rose Lutu Lawa. 

Maafisa Bima tawi la Dodoma wakifuatilia mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji akizungumza na maafisa wa Bima tawi la Dodoma sambamba na MNkurugenzi wa Bima za maisha Bi. Rose Lutu Lawa (katikati) na Bw. Fadhil Kasira.


Bw. Ruta F. Kaijage akifuatilia mazungumzo sambamba na maafisa wa bima tawi la Dodoma wakifuatilia kwa umakini mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.




Maafisa bima wakipozi katika picha pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji alipotembelea tawi la Dodoma. 

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI ATEMBELEA TAWI LA MOROGORO

Jengo la NIC Morogoro kwa nje





Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga kabla ya kuanza kikao na wafanyakazi wa tawi la Morogoro.

Mkurugenzi wa Bima za Maisha na Pensheni Bi. Rose Lutu Lawa akijianda na kikao pamoja an wafanyakazi wa Bima tawi la Morogoro. 

Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIC Bi. Tabu S. Kingu akijiandaa kwa makini na kikao hicho.

Meneja tawi la Morogoro Bi. Neema Mhauka.



Maafisa wa Bima Tawi la Morogoro wakifuatilia kwa makini kikao hicho Kutoka kulia ni Mhasibu Msaidizi Bw. Osmond Haule, Dereva wa Morogoro Bw. Saidi Kika na Dereva wa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Madodi.

Mhasibu Mkuu wa Tawi la Morogoro Bw. Jorwa Mtani (kulia) sambamba na maafisa bima Fred Solomon (katikati) na Shakwanande Kwayu wakati kikao hicho.

Mkurugenzi wa Bima za maisha na Pensheni Bi. Rose Lutu Lawa akiongea na wafanyakazi wa tawi la Morogoro wakati wa ziara ya kaimu Mkurugenzi Mtendaji .



Kaimu mkurugenzi Mtendaji akizungumza na Wafanyakazi wa tawi la Morogoro wakati wa ziara yake kikazi  kanda ya kati.



Tuesday, May 19, 2015

MEDICARE INSURANCE POLICY


Shirika la Bima la Taifa Tanzania linatambua na kuthamini uhai na afya ya mteja na ndiyo maana tunaendelea kutoa huduma za afya na matibabu kwa wanachama wa NIC nchini kote. Chini ni maelezo kwa ufupi kuhusu huduma za bima ya afya.





Chini ni sehemu ambazo mwanachama anaweza kufika kwa ajili ya huduma ya matibabu zaidi.




Monday, May 18, 2015

USHIRIKIANO NI SILAHA


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga (katikati) akiwa katika mahojiano na mtangazaji wa TBC1 Bw. Marin Hassan Marin (kushoto) sambamba na Meneja tawi la Dodoma Bw. Lugano Stanton.


Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi NIC Bi. Flora Kasambala akimwelekeza jambo Afisa ununuzi NIC Bi. Esther Sanga. 

Afisa Bima za Maisha Bi. Highness Mongo (kushoto) akimwelekeza mteja mpya jinsi ya kujaza fomu kwa ajili ya huduma za bima ya Matibabu



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Bima za Maisha na Pensheni Bi. Rose Lutu Lawa (wa kwanza Kulia), Mkuu wa Ktengo cha Mahusiano Bi. Mwanaidi Shemweta (wa kwanza kushoto) sambamba na mtangazaji wa kituo cha runinga TBC1 Marin Hassan Marin, baada ya mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya NIC.
.

MKUTANO NA UBUNGO PLAZA LTD



kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga akisalimiana na  Mhasibu Msaidizi wa Ubungo Plaza Ltd Bw. Nyembo Kigombey kabla ya kuanza mkutano, katikati ni Afisa Mtendaji wa Ubungo Plaza Ltd, Bw. Harun Mgude. 

Afisa Mtendaji wa Ubungo Plaza Ltd Bw. Harun Mgude akiwa katika picha ya pamoja na Mhasibu wa Ubungo Plaza Ltd Bw. Lihami Masoli.

Afisa Mtendaji wa Ubungo Plaza Limited Bw. Harun Mgude sambamba na mjumbe wa mkutano Bw. Pauline Gunje, wakiangalia mission na vision za NIC walipotembelea makao makuu makuu ya NIC kwa ajili ya mkutano.. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga akiwa na wajumbe wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa NIC makao makuu.