Monday, May 18, 2015

USHIRIKIANO NI SILAHA


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga (katikati) akiwa katika mahojiano na mtangazaji wa TBC1 Bw. Marin Hassan Marin (kushoto) sambamba na Meneja tawi la Dodoma Bw. Lugano Stanton.


Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi NIC Bi. Flora Kasambala akimwelekeza jambo Afisa ununuzi NIC Bi. Esther Sanga. 

Afisa Bima za Maisha Bi. Highness Mongo (kushoto) akimwelekeza mteja mpya jinsi ya kujaza fomu kwa ajili ya huduma za bima ya Matibabu



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Bima za Maisha na Pensheni Bi. Rose Lutu Lawa (wa kwanza Kulia), Mkuu wa Ktengo cha Mahusiano Bi. Mwanaidi Shemweta (wa kwanza kushoto) sambamba na mtangazaji wa kituo cha runinga TBC1 Marin Hassan Marin, baada ya mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya NIC.
.

MKUTANO NA UBUNGO PLAZA LTD



kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga akisalimiana na  Mhasibu Msaidizi wa Ubungo Plaza Ltd Bw. Nyembo Kigombey kabla ya kuanza mkutano, katikati ni Afisa Mtendaji wa Ubungo Plaza Ltd, Bw. Harun Mgude. 

Afisa Mtendaji wa Ubungo Plaza Ltd Bw. Harun Mgude akiwa katika picha ya pamoja na Mhasibu wa Ubungo Plaza Ltd Bw. Lihami Masoli.

Afisa Mtendaji wa Ubungo Plaza Limited Bw. Harun Mgude sambamba na mjumbe wa mkutano Bw. Pauline Gunje, wakiangalia mission na vision za NIC walipotembelea makao makuu makuu ya NIC kwa ajili ya mkutano.. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga akiwa na wajumbe wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa NIC makao makuu. 

KURUGENZI YA FEDHA IKIWA KATIKA MAPUMZIKO

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bi. Anne Mbughuni akiwaongoza kurugenzi ya Fedha na Utawala walipotembelea Nyumba ya makumbusho wilaya ya Bagamoyo. 

Mkurugenzi wa Fedha Bi. Anne Mbughuni akiwa katika picha ya pamoja na kurugenzi ya fedha, walipotembelea majumba ya makumbusho wilayani Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bi Anne Mbughuni pamoja na Meneja Rasilimali Watu Bw. Godbless Uronu wakipumzka baada ya mzunguko wa kutembelea makumbusho.

Baadhi ya wajumbe wa Kurugenzi ya Fedha NIC wakiangalia vitu vya asili.



Wakipozi katika picha ya pamoja kando ya bahari







Thursday, May 14, 2015

KUMBUKUMBU

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bi Anne Mbughuni akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha mahusiano Bi Mwanaidi Shemweta na Ntiba Bunny 

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Bw. Henry Machoke akiwa katika mradi wa kuelimisha wanafunzi juu ya elimu ya Bima.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Justine P. Mwandu akipozi katika picha ya pamoja na wakurugenzi, menejiment na wakuu wa idara. 

Alieyekuwa Mkurugrnzi Mtendaji Bw. Justine P. Mwandu akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hati ya bima ya matumaini wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mahusiano Bi. Mwanaidi Shemweta, Mkurugenzi wa Bima za maisha na Pensheni Bi. Rose Lutu Lawa. 

MEI MOSI 2015

Wafanyakazi wa NIC wakiwa tayari kwa maandamano kuelekea uwanja wa |Taifa Dar es Salaam. 

Pichani juu na chini wafanayakazi wakishiriki katika maandamano Uwanja wa Taifa





Gari la matangazo kwa ajili ya wafanyakazi wa NIC



Mgeni rasmi katika siku ya wafanyakazi duniani amabaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, akiingia ukumbini kwa muziki uliokuwa umeandaliwa na wafanyakazi kumuunga mkono kwa kuserebuka.

Mgeni rasmi akicheza muziki na wafanyakazi wa NIC

NIC IKIWAKILISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Baadhi ya wafanyakazi wa NIC wakiwa katika maandamano siku ya wanawake duniani 2015. 

Washiriki wa maandamano katika picha ya pamoja na wajasiriamali jijini Dar es Salaam.

Washiriki wa maandamano wakiwa katika pozi 

Mkuu wa kitengo cha mahusiano akiwa katika picha ya pamoja na waandaji wa maandamano ya wajariamali kutoka Mentoring Walk.org.

MSAADA KWA JAMII NI MOJA YA HUDUMA KUTOKA NIC

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe Gulam Hafeez akikagua vifaa vya watoto wenye ulemavu wa Ngozi, Wasioona na kusikia baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NIC tawi la Shinyanga Bi Halima Makange.

Meneja wa NIC Tawi la Shinyanga Bi Halima Makange akitoa vifaa vya huoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi, wasioona na kusikia cha Buhangija Shinyanga, anayepokea msaada huo ni Msimamizi wa kituo hicho Mwl Peter Ajali.

Meneja Wa NIC Tawi la Shinyanga Bi Halima Makange akimuonesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe Gulam Hafeez vifaa vya watoto wenye ulemavu wa Ngozi, wasioona na kusikia katikati ni Mlezi wa Kituo hicho Mwl Peter Ajali Akishuhudia .

Mtaalamu wa Macho Fani ya Uoni hafifu kutoka Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr. Ntoke Sospeter Wilson akiwaelezea watoto hao namna ya kutumia darubini Kiona Mbali.

Meneja wa NIC Tawi la Shinyanga akiwa katikati ya watoto wenye ulemavu wa Ngozi wa ngozi, wasioona na kusikia wakiwa wakijaribu kutumia kifaa cha Darubini Kiona Mbali katika kituo hicho Mjini Shinyanga.