Monday, March 23, 2015

MKUTANO WA WAFANYAKAZI ULIOITISHWA NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI.


Shirika la Bima la Taifa Tanzania limetoa rai juu ya kutowafumbia macho wafanyakazi wazembe na wavivu ambao hawatakuwa tayari kufanya kazi kwa kujituma na ufanisi kwa ajili ya kuliletea Shirika maendeleo hususani kipindi hiki cha ushindani wa biashara katika soko la Bima.

Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga mwishoni mwa wiki alipoitisha mkutano na wafanyakazi wa shirika wa Makao Makuu pamoja na matawi yaliyopo Dar es Salaam ili kujadili nao masuala yanayohusu shirika.

"Nitakuwa na 'zero tolerance' kwa wafanyakazi wavivu na wasionea huruma shirika, tusomee teknolojia ili kuongeza ufanisi katika utendaji wetu wa kazi, pia naomba turekebishane kwenye mapungufu, tuchape kazi, tusaidiane katika kuliletea shirika maendeleo naamini tunahitaji mengi, mishahara ni midogo tuongeze juhudi ili kuongeza mishahara." Alisisitiza Kamanga.

Kamanga aliongeza, "Nataka tuendeshe shirika kibiashara zaidi, NIC imebahatika kuwa na wataalamu wengi kuzidi mashirika mengine, nimeunda kikosi maalum kitakachoongozwa na Bw. Chaina Chacha. tuvute soksi, tukaze mikanda, tuongeze juhudi, tusikae sana kwenye viti tuchape kazi, tuongeze tija tutaona mafanikio."

Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki ukiwa na lengo la kukutanisha Kurugenzi, Idara na wafanyakazi wa NIC wa Dar es Salaam wa Makao Makuu ya Shirika kwa lengo la kujadili na kuwekana sawa kuhusu maendeleo na marekebisho yanayotakiwa ndani ya Shirika la Bima la Taifa.

Wajumbe waliohudhuria mkutano wakifuatilia kwa makini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (watatu kutoka kushoto) akiongea na wafanyakazi wa NIC.
Wajumbe wakifuatilia kwa umakini mkutano.

No comments: