Monday, March 30, 2015

NIC YAENDELEZA MAFUNZO KWA WANACHAMA WA TARWOTU MOROGORO.



NIC kwa kushirikiana na TARWOTU imeendelea kutoa elimu nchini kwa mawakala,madereva, makondakta, na matingo nchini ili waweze kutambua haki zao hususani mishahara, mikataba ya kazi, malipo, likizo ya mwaka kama wafanyakazi wengine na masaa malum ya kufanya kazi, na wiki iliyopita ilikuwa ni zamu ya wakazi wa Morogoro ambao walipata nafasi ya kuuliza maswali.

Mgeni rasmi Eng. Evarist Ndikilo alisema,"Ukiacha Ukimwi na Malaria, ajali ndiyo zinachangia sana vifo vya ajali hapa nchini, nawahamasisha wote mjikatie Bima kwa ajili ya maisha yenu ya sasa na ya baadae. Nawaomba mjikatie kinga kwa ajili yenu na familia zenu kwa ujumla."

Eng. Ndikilo Aliongeza kuwa ni muhimu polisi kuchukua hatua kwa kuhakikisha kila dereva hususani wa bodaboda awe na leseni na kuwataka kuwafichua ambao hawana leseni kwani wao ndiyo wanawajua madereva awenzao ambao hawana leseni tofauti na polisi wa usalama barabarani.

Naye katibu wa TARWOTU Bw. Salim Abdallah akisoma risala yake kwa mgeni rasmi alisema kuwa wizi wa kuporwa pikipiki na kuuawa kinyama kwa madreva hususani wa bodaboda unatakiwa uchukuliwe hatua na serikali. Pia alisema bado wanaendelea na nia ya chama ya kuunganisha madereva na kuwawezesha kutambua haki zao za msingi bila uoga.


Mwakilishi wa mgeni rasmi Bw. Noel Kazimoto akizungumza katika mkutano uliofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki, akizungumza na wanachama mbalimbali walihudhuria mkutano.


Wanachama wa TARWOTU wakifuatilia kwa makini mafunzo waliyokuwa wakipata kutoka kwa watoa mada mabalimbali.


Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja wa NIC,  Bw. Henry Machoke akiongea na wanachama wa TARWOTU.

Mkurugenzi wa Bima za Maisha na Pensheni wa NIC B i. Rose Lutu Lawa (katikati) akiwa pamoja na mwenyekiti wa (TARWOTU) Bw. Shukuru Mlawa (kushoto) na Afisa wa SUMATRA.

Bi. Rose Lutu Lawa akizungumza na wanachama wa TARWOTU waliohudhuria mkutano.

HISTORY: Chama cha wafanyakazi wa usafirishaji kwa njia ya Barabara Tanzania (TARWOTU) kilianzishwa mwaka 2010 baada ya migogoro ya madereva wa Dar es Salaam na Mbeya kudai haki zao za (BIMA na NSSF) kutoka kwa waajiri wao, na kilipata usajiri rasmi 21 Januari 2013.

No comments: