Monday, March 30, 2015

NIC YAENDELEZA MAFUNZO KWA WANACHAMA WA TARWOTU MOROGORO.



NIC kwa kushirikiana na TARWOTU imeendelea kutoa elimu nchini kwa mawakala,madereva, makondakta, na matingo nchini ili waweze kutambua haki zao hususani mishahara, mikataba ya kazi, malipo, likizo ya mwaka kama wafanyakazi wengine na masaa malum ya kufanya kazi, na wiki iliyopita ilikuwa ni zamu ya wakazi wa Morogoro ambao walipata nafasi ya kuuliza maswali.

Mgeni rasmi Eng. Evarist Ndikilo alisema,"Ukiacha Ukimwi na Malaria, ajali ndiyo zinachangia sana vifo vya ajali hapa nchini, nawahamasisha wote mjikatie Bima kwa ajili ya maisha yenu ya sasa na ya baadae. Nawaomba mjikatie kinga kwa ajili yenu na familia zenu kwa ujumla."

Eng. Ndikilo Aliongeza kuwa ni muhimu polisi kuchukua hatua kwa kuhakikisha kila dereva hususani wa bodaboda awe na leseni na kuwataka kuwafichua ambao hawana leseni kwani wao ndiyo wanawajua madereva awenzao ambao hawana leseni tofauti na polisi wa usalama barabarani.

Naye katibu wa TARWOTU Bw. Salim Abdallah akisoma risala yake kwa mgeni rasmi alisema kuwa wizi wa kuporwa pikipiki na kuuawa kinyama kwa madreva hususani wa bodaboda unatakiwa uchukuliwe hatua na serikali. Pia alisema bado wanaendelea na nia ya chama ya kuunganisha madereva na kuwawezesha kutambua haki zao za msingi bila uoga.


Mwakilishi wa mgeni rasmi Bw. Noel Kazimoto akizungumza katika mkutano uliofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki, akizungumza na wanachama mbalimbali walihudhuria mkutano.


Wanachama wa TARWOTU wakifuatilia kwa makini mafunzo waliyokuwa wakipata kutoka kwa watoa mada mabalimbali.


Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja wa NIC,  Bw. Henry Machoke akiongea na wanachama wa TARWOTU.

Mkurugenzi wa Bima za Maisha na Pensheni wa NIC B i. Rose Lutu Lawa (katikati) akiwa pamoja na mwenyekiti wa (TARWOTU) Bw. Shukuru Mlawa (kushoto) na Afisa wa SUMATRA.

Bi. Rose Lutu Lawa akizungumza na wanachama wa TARWOTU waliohudhuria mkutano.

HISTORY: Chama cha wafanyakazi wa usafirishaji kwa njia ya Barabara Tanzania (TARWOTU) kilianzishwa mwaka 2010 baada ya migogoro ya madereva wa Dar es Salaam na Mbeya kudai haki zao za (BIMA na NSSF) kutoka kwa waajiri wao, na kilipata usajiri rasmi 21 Januari 2013.

Thursday, March 26, 2015

MKUTANO WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA BARABARA TANZANIA (TAROTWU).



Chama cha Wafanyakazi wa Usafirishaji kwa njia ya Barabara Tanzania (TAROTWU) kesho kitakuwa na mkutano muhimu kwa ajili ya madereva wa mabasi ya abiria yaendayo mkoani na vijijini pamoja na vitongoji vya Manispaa ya Morogoro, madereva wa malori,bajaji na pikipiki, makondakta,matingo na mafundi wa magari na maajenti wa mabasi na malori.

Katika mkutano huo kutakuwa na mada elimu kutoka kwa Shirika la Bima la Taifa, SUMATRA, TRA na AFISA KAZI wa MOROGORO, Mnaombwa kufika bila kukosa kuhudhuria mkutano huu muhimu katika kazi zetu za kila siku utakaofanyika kesho tarehe 27 Januari 2015 katika ukumbi wa MOUNT ULUGURU.

Fika bila kukosa ili ufaidike na unufaike kwa elimu utakayopata, HAKUNA KIINGILIO.

Tuesday, March 24, 2015

MOTOR INSURANCE GUIDANCE

Karibu NIC ujipatie huduma za Bima ya Magari kama picha chini zinavyojieleza. Karibu tukuhudumie.


Ni Bima za magari zinazotolewa na NIC kwa ajili ya kinga dhidi ya ajali za barabarani, moto, wizi, majeraha ama vifo endapo vitatokea basi muathirika au familia itapata fidia kulingana na ukubwa wa bima iliyokatwa. Bima hizi hutolewa kwa aina zote za magari pamoja na pikipiki za kawaida na zile za magurudumu matatu (kama bajaji). 


Mawasiliano: Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii ya Bima, tafadhali tembelea katika tawi lililo karibu na wewe kwa msaada zaidi;



Picha hapo juu ni maelekezo juu ya Bima za Magari zinvyopatikana hapa NIC, kwa maelezo na ushauri juu ya huduma zetu, wasiliana nasi kwa mawasiliano hapo juu.





TAHADHARI: MVUA KUBWA KUENDELEA KUNYESHA KUANZIA MACHI 23-25 KWENYE MAENEO YA PWANI YA NCHI.


Monday, March 23, 2015

MAFUNZO YA BIMA KWA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA BARABARA TANZANIA (TAROTWU).


Chama cha wafanyakazi wa usafirishaji kwa njia ya barabara Tanzania (TAROTWU) kimeweka mkakati wa kuhakikisha kwamba wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji wanapewa elimu juu ya Bima na kuhamasishwa kukata Bima ya ajali ili kujiwekea kinga. 

TAROTWU ikiwasilisha risala yao kwa mgeni rasmi Rose Lutu Lawa,  ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) chama hicho kilisema mkakati wao ni kuhakikisha wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji wananufaika na kupata maslahi bora ili kuondokana na matatizo yanayotokana na changamoto zilizopo katika soko la utandawazi na kuimarisha uchumi wa Taifa.

Waliongeza kuwa mkakati wao pia ni kuunda kamati za Elimu kila mkoa ili zishirikiane na idara ya kazi, CMA, SUMATRA, BIMA NIC na vyuop vya VETA nchini na wadau wengine katika kuelimisha wafanyakazi wakiwemo madereva malori, mabasi ya abiria, bodaboda, bajaji, mafundi wa magari na makondakta, mawakala wa mabasi na malori ya mizigo na mautingo 

Mgeni rasmi katika mafunzo hayo alikuwa mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji  wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bi. Rose Lutu Lawa (watatu kushoto). 

Mr. Mabula akifungua mkutano maalum wa wafanyakazi katika ukumbi wa chuo cha VETA Dodoma tarehe 19/03/2015.


Wanachama wa TAROTWU wakifuatilia mafunzo.






MKUTANO WA WAFANYAKAZI ULIOITISHWA NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI.


Shirika la Bima la Taifa Tanzania limetoa rai juu ya kutowafumbia macho wafanyakazi wazembe na wavivu ambao hawatakuwa tayari kufanya kazi kwa kujituma na ufanisi kwa ajili ya kuliletea Shirika maendeleo hususani kipindi hiki cha ushindani wa biashara katika soko la Bima.

Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga mwishoni mwa wiki alipoitisha mkutano na wafanyakazi wa shirika wa Makao Makuu pamoja na matawi yaliyopo Dar es Salaam ili kujadili nao masuala yanayohusu shirika.

"Nitakuwa na 'zero tolerance' kwa wafanyakazi wavivu na wasionea huruma shirika, tusomee teknolojia ili kuongeza ufanisi katika utendaji wetu wa kazi, pia naomba turekebishane kwenye mapungufu, tuchape kazi, tusaidiane katika kuliletea shirika maendeleo naamini tunahitaji mengi, mishahara ni midogo tuongeze juhudi ili kuongeza mishahara." Alisisitiza Kamanga.

Kamanga aliongeza, "Nataka tuendeshe shirika kibiashara zaidi, NIC imebahatika kuwa na wataalamu wengi kuzidi mashirika mengine, nimeunda kikosi maalum kitakachoongozwa na Bw. Chaina Chacha. tuvute soksi, tukaze mikanda, tuongeze juhudi, tusikae sana kwenye viti tuchape kazi, tuongeze tija tutaona mafanikio."

Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki ukiwa na lengo la kukutanisha Kurugenzi, Idara na wafanyakazi wa NIC wa Dar es Salaam wa Makao Makuu ya Shirika kwa lengo la kujadili na kuwekana sawa kuhusu maendeleo na marekebisho yanayotakiwa ndani ya Shirika la Bima la Taifa.

Wajumbe waliohudhuria mkutano wakifuatilia kwa makini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (watatu kutoka kushoto) akiongea na wafanyakazi wa NIC.
Wajumbe wakifuatilia kwa umakini mkutano.

Thursday, March 19, 2015

NIC SASA KWENYE MKONGO WA TAIFA.

Mameneja wa mradi kutoka TTCL na wa NIC wakiwa na tabasamu baada ya kukamilisha mradi huo.


Mkrugenzi wa Fedha wa NIC Bi. Anne Mbughuni akifuatilia mradi huo kwenye picha.




Picha ikionyesha matawi ya NIC yaliyounganishwa kwenye mtandao wa TTCL (MPLS-VPN)

Mkuregenzi Mtendaji Mstaafu Bw. Justine Mwandu akipokea cheti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr. Kamugisha Kazaura

Menejimenti ya NIC na TTCL katika picha ya Pamoja baada ya kukamilika kwa mradi wa Mkongo wa Taifa.

MKUTANO WA SEMINA ELEKEZI ULIOITISHWA NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI KWA MENEJIMENTI YA SHIRIKA

Wajumbe wa semina elekezi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa semina.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Sam Kamanga akizungumza na wajumbe walioshiriki semina elekezi (hawapo pichani)

Wajumbe walioshirikisemina elekezi wakipozi kwa picha ya ukumbusho mara baada ya kumalizika kwa semina elekezi iliyoitishwa na kaimu Mkurugenzi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga (kushoto) akipozi katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dr. Edmund Mndolwa. 

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dr. Edmund Mndolwa, Mkurugenzi wa masoko Bw. Henry Machoke na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Sam Kamanga wakipozi mara baada ya kumalizika kwa semina elekezi.







NDOTO YA KUSIMIKA TEKNOLOJIA MPYA YA TEHAMA KWA SHIRIKA LA BIMA YAKAMILIKA


Watalaam wa Bima za Maisha na Bima zisizo za maisha Bw. Lazaro Bangilana (Kushoto) na Isihaka Kibamba (Kulia) wakipeana maelekezo juu a Teknolojia mpya ya BIMA ambayo imeanza kutumika kwa majaribio kwenye shirika la Bima la Taifa


Kaimu kiongozi (ag. Project Manager) Mr . Samson Lugembe akifuatilia kwa karibu akiwa na wataalam kutoka nje majaribio ya Teknolojia ya Teama kwa upande wan bima zisizo za maisha.