Kikao cha bunge kimeahirishwa hadi kesho saa 3 Asubuhi kutokana
na msiba wa Mbunge wa Geita (CCM),
Donald Max (58) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa mbunge huyo
(pichani) alifariki jana saa 12.00 jioni katika hospitali hiyo.Ndugai alisema
Max alikuwa mahututi kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita na mwili
wa marehemu unatarajiwa kuzikwa Jumamosi Juni 27 jijini Dar es salaam.
Max alizaliwa Mei 22 mwaka 1957 na kusoma katika Shule ya Msingi
ya Salvatorian Convent na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari ya Azania
mwaka 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1980 alikwenda nchini Urusi na kusoma kozi ya ufundi
katika Chuo cha Ufundi cha Roston on Don kabla ya kujiunga na Taasisi ya
Volgograd Polytechnical nchini humo na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika
Uhandisi.
Mungu ampumzishe mahali pema peponi.
No comments:
Post a Comment