Wednesday, April 22, 2015

BIMA YA KINGA YA MAGARI YA BIASHARA



BIMA YA KINGA YA MAGARI YA BIASHARA.

Ununuzi wa gari la biashara kwa hakikia ni mojawapo ya uwekezaji mkubwa kifedha unaofanywa na taasisi ya biashara iwe ya biashara ya mtu mmoja au shirika kubwa.
Sisi NIC tunatambua huli na kwa uangalifu tumekuandalia Bima ya kinga ya Magari ya biashara ili kulinda uwekezaji huu.

FAIDA ZA BIMA HII

Bima  kubwa (Comprehensive) 

Chini ya bima jumuishi tunatoa kinga iwapo gari lako na vifaa vyake pamoja na vipuri vitaibwa au kuharibika. Gari lako linapokuwa katika biashara ya magari, kinga ya kawaida itaendelea. Gharama za kukokota gari likipata ajali hadai sehemu ya kuaminika ya matengenezo zitarejeshwa kwa kiwango kischozidi shilingi TShs 50,000/=. Mwenye gari unaweza kuidhinisha matengenezo ya hilo gari la biashara ili mradi unatujulisha mapema na gharama zisizidi TShs 1,500,000/=.



Bima ya muathirika mwingine (Third Party).

Kinachojumuishwa moja kwa moja katika Bima yako ya Kinga ya Magari ya Biashara ni ahadi yetu ya kulipa madai halali yanayoelekezwa kwako na watu wengine ambao wewe au dereva wako mlio kwenye bima hii mmewasababisha madhara ya uharibifu au maumivu. Kinga ya kifedha kwa kusababisha maumivu kwa watu wengine haina ukomo na hata uharibifu kwa mali za watu wengine kiwango chake kinafikia hadi TShs 10,000,000/=. 

Kukokota

Bima hii inakukinga pia unapokokota trela au gari lingine ambalo halijiendeshi lenyewe.


Punguzo kama hakuna madai.

NIC itakuzawadia kwa uendeshaji wa makini unaoepusha ajali kwa punguzo la kiwango cha juu kuliko ilivyowahi kutokea. Kwa mfano asilimia 10 (10%) baada ya mwaka mmoja tu usiokuwa na madai, hadi kufikia asilimia 30 (30%) baada ya miaka mitano.

Mawasiliano:
Kwa maelezo zaidi juu ya bima unayoweza kupata kwa viwango nafuu uliza katika tawi letu lolote au kwa mawakala wetu wenye uzoefu.


No comments: