Wednesday, February 6, 2013

Uteuzi....

Uongozi wa shirika la bima la taifa NIC umemteua Bi. Tabu Kingu kukaimu nafasi ya Mhasibu Mkuu wa shirika nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gregory Ngonyani ambaye anakwenda kujiunga na Tanzania Reinsurance Corporation (TAN-RE). Uteuzi huu umeanza kutoka tarehe 5/02/2013.

Uongozi  umetoa shukrani nyingi kwa Bw. Ngonyani kwa kulitumikia shrika kwa kipindi chote alichokuwa katika ajira kama Mhasibu Mkuu.


Bi Tabu Kingu akiwa anasisitizia jambo katika moja ya mikutano
ya menejimenti ya shirika la Bima la Taifa (NIC)


Bi. Tabu Kingu akiwa na Mameneja wa matawi ya shirika la Bima
Kutoka kushoto ni Bw. Ignatius Iruganyuma (Musoma),
Bi. Halima Makange (Shinyanga), Bi. Neema Mhauka (Morogoro)
 na Bi.Catherine Magodi (Life House-Dar Es Salaam).

No comments: