Wednesday, June 24, 2015

MBUNGE WA GEITA AFARIKI DUNIA.





Kikao cha bunge kimeahirishwa hadi kesho saa 3 Asubuhi kutokana na msiba wa  Mbunge wa Geita (CCM), Donald Max (58) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa mbunge huyo (pichani) alifariki jana saa 12.00 jioni katika hospitali hiyo.Ndugai alisema Max alikuwa mahututi kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita na mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa Jumamosi Juni 27 jijini Dar es salaam. 
Max alizaliwa Mei 22 mwaka 1957 na kusoma katika Shule ya Msingi ya Salvatorian Convent na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari ya Azania mwaka 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1980 alikwenda nchini Urusi na kusoma kozi ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Roston on Don kabla ya kujiunga na Taasisi ya Volgograd Polytechnical nchini humo na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uhandisi.
Mungu ampumzishe mahali pema peponi.

Tuesday, June 9, 2015

CHUKUA TAHADHARI: POLIS IRINGA YAKAMATA DVD ZA MAFUNZO YA KIGAIDI.



Polisi Iringa yakamata DVD za mafunzo ya kigaidi


Jeshi la polisi mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo ya kijeshi yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al shaabab cha nchini Somalia.
Baadhi ya DVD zilizokamatwa
Jeshi la polisi mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo ya kijeshi yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al shaabab cha nchini Somalia zilizokuwa zikitumika na watoto wa mitaani wanaodaiwa kuwa walikuwa wakichukua mafunzo kwakutumia DVD hizo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari akieleza kuwa mikanda hiyo ilikuwa ikitumiwa na vijana hao wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16 inaonesha ukatili na mauaji yanayodaiwa kufanywa na kikundi cha kigaidi cha Al shaabab mikanda ambayo walikuwa wakiitazama kwa kutumia kompyuta mpakato yaani laptop.
Aidha kamanda Mungi amesema pamoja na mikanda hiyo ya DVD pia jeshi hilo limekamata watu wawili wanaojihusisha na biashara ya bangi wakiwa na magunia matatu ya bangi katika harakati za kufunga bangi hiyo kwenye vifurushi vidogo tayari kuisambaza kwa wateja wao.
Mungi ameongeza kuwa kamata kamata hiyo iliyofanywa na jeshi hilo mkoa wa Iringa pia imekamata nguzo 35 za umeme za shirika la umeme nchini TANESCO, nyaya za kusambaza umeme na vifaa vingine zikiwa zimehifadhiwa kwa watu binafsi wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za kiupelelezi.

Monday, June 8, 2015

UANDIKISHAJI WAPIGA KURA



Tume ya Taifa ya Uchaguzi yasema imevuka malengo ya uandikishaji wapiga kura katika mikoa ya kusini ambapo mkoani Lindi wameandikishwa 569,261, Ruvuma 826,779, Iringa walioandikishwa ni 526,006 na Mtwara walioandikishwa ni 682, 295. Himahima "Mfanyakazi jiandikishe, kura yako inathamani kwa maendeleo yetu".

Tuesday, June 2, 2015

TANZIA


Mbunge wa jimbo la Ukonga Dar es Salaam kupitia tiketi ya (CCM) Eugine Mwaiposa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini nyumbani kwake Dodoma.
Kwa mujibu wa Naibu Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai ambaye amelitangazia bunge leo majira ya saa 7 mchana, marehemu Mwaiposa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu.
Ndugai amesema kuwa kwa sasa msiba upo nyumbani kwake eneo la Chadulu Dodoma ambapo pia familia yake inasubiria hapo kwa ajili ya kuaga mwili wake shughuli ambayo itafanyika kesho (Jumatano).
Bunge limeahirishwa hadi keshokutwa saa 3 Asubuhi.
Mungu ametoa Mungu ametwaa jina lake lihimidiwe. R.I.P

USALAMA BARABARANI


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza, Mohamed Likwata akizungumza na wasafiri waliokuwa wakielekea Bukoba, kwenye Kituo cha Mabasi Nyegezi jana, wakati wa kampeni ya “Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” kupitia namba 0800757575 bure, kampeni inayoendeshwa kwa pamoja kati ya Vodacom Tanzania, Jeshi hilo na vituo vya ITV/Redio One. Kampeni hiyo ilibuniwa kuwadhibiti madereva wakorofi wasiozingatia sheria za usalama barabarani wakiwa safarini. 
Baadhi ya picha za ajali mbaya zilizowahi kutokea nchini Tanzania na kupoteza uhai wa wananchi.