Wednesday, January 6, 2016

HONGERENI

 
Tukiwa tumefanikiwa kuumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, Shirika la Bima la Taifa Tanzania linapenda kuchua nafasi hii kuwapongeza wafanyakazi hawa waliojaaliwa kufunga pingu za maisha ndani ya 2015, Pongezi za dhati kwao Bi Faith Robert, Bi Hajra Kadry, Bw. Juma Ayubu, Bw. Juma Kiungulia, Nasson Mwandumbya na Bw. Daniel Manupa. Tunawatakia maisha mema na baraka tele katika maisha yenu ya ndoa.
 
 
Bwana Juma Ayoub akiwa na mke wake wakati wa tafrija ya sherehe ya ndoa yao.

Bi. Faith Robert akiwa na mumewe mara baada ya kufunga pingu za maisha jijini Dar es Salaam.

Bi. Hajra Kadry akiwa na mumewe wakati wa tafrija ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Bw. Juma Kiungulia akiwa katika picha ya pamoja na mke wake na  wafanyakazi wa NIC wakati wa tafrija ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaa.

Bw. Daniel Manupa na mkewe wakila kiapo cha ndoa yao.

Bw. Nasson Mwandumbya na mkewe wakiwa na nyuso za furaha wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Monday, December 21, 2015

BIMA YA UJENZI (CONTRACTOR'S ALL RISKS)




BIMA YA UJENZI (CONTRACTOR'S ALL RISKS)
Bima hii inatoa kinga ya ujenzi wa majengo, barabara, madaraja, n.k. dhidi ya uharibifu wa kitu kinachojengwa. Performance Bonds, na advance payments bonds ni bima zinazotoa dhamana kwa mkandarasi, atafanya kazi yake ya ujenzi kadri ya mkataba unavyoelekeza. Fika katika ofisi za NIC upate huduma hii.

Tuesday, October 6, 2015

HUDUMA KWA JAMII - NIC YAALIKWA KWENYE MAHAFALI YA 32 YA KIDATO CHA NNE KWENYE SHULE YA WASICHANA KIFUNGILO, LUSHOTO MKOANI TANGA



 MGENI RASMI KAIMU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA BIMA BW. SAM KAMANGA AKITAMBULISHWA RASMI KWA WAGENI WAALIKWA.


  
MGENI RASMI KAIMU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA BIMA 
                               BW. SAM KAMANGA AKIHUTUBIA WAGENI WAALIKWA


                             MGENI RASMI KAIMU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA BIMA 
                                 AKIWAZAWADIA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI 
                                                WA KIDATO CHA 4 "CLASS OF 2015"






 
      MGENI RASMI KAIMU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA BIMA AKITOA SHUKRANI





                              MGENI RASMI KAIMU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA BIMA 
                                 AKIWAZAWADIA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI 
                                                WA KIDATO CHA 4 "CLASS OF 2015"








PICHA YA PAMOJA NA WANAFUNZI "CLASS OF 2015" 
KIFUNGILO GIRLS





NIC YASHIRIKI 18th INSURANCE DAY 2015