WAZIRI WA FEDHA MH. SAADA MKUYA SALUM (MBUNGE)
HAPA TUNAKULETEA SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA ALIPOGUSIA MASUALA YA BIMA NA MUSTAKABALI WA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC)
Huduma za Bima
Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za
Bima – TIRA
99. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia
Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima imekamilisha na kutoa Mkakati wa
Kuendeleza Bima ya Watu wa Kipato cha Chini - National Micro Insurance Strategy
2014-2017. Aidha, hadi kufikia Aprili 2014, kampuni 30, madalali 100 na
mawakala 500 wa bima alisajiliwa. Vile vile, mauzo ya bima yaliongezeka kutoka
shilingi bilioni 406.7 mwaka 2012/13 hadi kufikia shilingi bilioni 481.7 sawa
na ongezeko la asilimia 18.5.
100. Mheshimiwa Spika, katika mwaka
2014/15,
TIRA
inatarajia kutekeleza yafuatayo: kuendelea na maandalizi ya kufungua ofisi
nyingine za kanda;kuendelea na utaratibu wa uoanishaji sheria na kanuni za soko
la bima katika eneo la Afrika Mashariki na lile la nchi za SADC; kuendelea na
tafiti za bima ya kilimo, mifugo, pamoja na bima za watu wa kipato cha chini; na
kukamilisha taratibu za kuanzisha bima ya Takaful.
Shirika la Bima la Taifa – NIC
101.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara ilikamilisha urekebishaji wa
Shirika la Bima la Taifa na usimikaji wa mfumo wa TEHAMA kwa lengo la kuongeza
ufanisi. Utendaji wa Shirika kibiashara uliendelea kuimarika ambapo mapato ya
bima yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 27.38 mwaka 2012, hadi kufikia
shilingi bilioni 31.53 mwaka 2013, ongezeko hilo ni sawa na asilimia 15. Mapato
haya yalitokana na makusanyo ya bima za mtawanyo, vitega uchumi na mapato
mengine.
102. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia
Desemba 2013, NIC ililipa madai ya wateja ya shilingi bilioni 8.31. Malipo hayo
yalilipwa kwa wateja wa bima za maisha kiasi cha shilingi bilioni 5.71 na
wateja wa bima za kawaida kiasi cha shilingi bilioni 2.60.
103. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15,
Wizara itaendelea na mkakati wa kuligawa Shirika katika kampuni mbili, ambayo
ni Kampuni ya Bima za Maisha na Kampuni ya Bima za Kawaida. Aidha, Shirika
litaendelea na mkakati wa kujitangaza zaidi na kuongeza biashara kwa kubuni
bima mpya zinazokidhi mahitaji ya wananchi.
Kwa kusoma hotuba yote nenda kwenye muelekeo huu;
source: Ministry of Finance
No comments:
Post a Comment