Friday, June 27, 2014

MKURUGENZI MTENDAJI NA MAOFISA WA JUU WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA TEHAMA GENISYS CONFIGURATOR

Mkurugenzi Mtendaji  na timu yake amaliza kupata maelekezo ya mwisho juu ya mfumo mpya TEHAMA unavyofanya kazi.


(Kutoka kushoto kwenda kulia)

Mkurugenzi Mtendaji Bw. Justine Mwandu, Bw. Gosbert Kafanabo Mkuu wa Idara ya Ukaguzi wa mahesabu ya ndani , Bw. Deepak Mtaalam wa Mtambo mpya wa TEHAMA kutoka India ,
Bi. Anne Mbughuni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Hamza Ngereza (Mwanafunzi katika majaribio) Msaidizi idara ya TEHAMA na Bw. Mohamed Rashid Mtaalamu wa ndani wa  mfumo mpya wa
TEHAMA  GENISYS CONFIGURATOR

Friday, June 6, 2014

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MH. SAADA MKUYA SALUM (MBUNGE) ALIYOIWASILISHA BUNGENI AKIWASILISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA KWA MWAKA 2014/15

WAZIRI WA FEDHA MH. SAADA MKUYA SALUM (MBUNGE)

HAPA TUNAKULETEA SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA ALIPOGUSIA MASUALA YA BIMA NA MUSTAKABALI WA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC)


Huduma za Bima

Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima – TIRA
99. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima imekamilisha na kutoa Mkakati wa Kuendeleza Bima ya Watu wa Kipato cha Chini - National Micro Insurance Strategy 2014-2017. Aidha, hadi kufikia Aprili 2014, kampuni 30, madalali 100 na mawakala 500 wa bima alisajiliwa. Vile vile, mauzo ya bima yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 406.7 mwaka 2012/13 hadi kufikia shilingi bilioni 481.7 sawa na ongezeko la asilimia 18.5.

100. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,
TIRA inatarajia kutekeleza yafuatayo: kuendelea na maandalizi ya kufungua ofisi nyingine za kanda;kuendelea na utaratibu wa uoanishaji sheria na kanuni za soko la bima katika eneo la Afrika Mashariki na lile la nchi za SADC; kuendelea na tafiti za bima ya kilimo, mifugo, pamoja na bima za watu wa kipato cha chini; na kukamilisha taratibu za kuanzisha bima ya Takaful.
  
Shirika la Bima la Taifa – NIC
101. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Wizara ilikamilisha urekebishaji wa Shirika la Bima la Taifa na usimikaji wa mfumo wa TEHAMA kwa lengo la kuongeza ufanisi. Utendaji wa Shirika kibiashara uliendelea kuimarika ambapo mapato ya bima yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 27.38 mwaka 2012, hadi kufikia shilingi bilioni 31.53 mwaka 2013, ongezeko hilo ni sawa na asilimia 15. Mapato haya yalitokana na makusanyo ya bima za mtawanyo, vitega uchumi na mapato mengine.
  

102. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Desemba 2013, NIC ililipa madai ya wateja ya shilingi bilioni 8.31. Malipo hayo yalilipwa kwa wateja wa bima za maisha kiasi cha shilingi bilioni 5.71 na wateja wa bima za kawaida kiasi cha shilingi bilioni 2.60.

103. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15, Wizara itaendelea na mkakati wa kuligawa Shirika katika kampuni mbili, ambayo ni Kampuni ya Bima za Maisha na Kampuni ya Bima za Kawaida. Aidha, Shirika litaendelea na mkakati wa kujitangaza zaidi na kuongeza biashara kwa kubuni bima mpya zinazokidhi mahitaji ya wananchi.

Kwa kusoma hotuba yote nenda kwenye muelekeo huu;

http://www.mof.go.tz/mofdocs/msemaji/MUHUTASARI%20WA%20HOTUBA.pdf

source: Ministry of Finance