Wednesday, January 6, 2016

HONGERENI

 
Tukiwa tumefanikiwa kuumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, Shirika la Bima la Taifa Tanzania linapenda kuchua nafasi hii kuwapongeza wafanyakazi hawa waliojaaliwa kufunga pingu za maisha ndani ya 2015, Pongezi za dhati kwao Bi Faith Robert, Bi Hajra Kadry, Bw. Juma Ayubu, Bw. Juma Kiungulia, Nasson Mwandumbya na Bw. Daniel Manupa. Tunawatakia maisha mema na baraka tele katika maisha yenu ya ndoa.
 
 
Bwana Juma Ayoub akiwa na mke wake wakati wa tafrija ya sherehe ya ndoa yao.

Bi. Faith Robert akiwa na mumewe mara baada ya kufunga pingu za maisha jijini Dar es Salaam.

Bi. Hajra Kadry akiwa na mumewe wakati wa tafrija ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Bw. Juma Kiungulia akiwa katika picha ya pamoja na mke wake na  wafanyakazi wa NIC wakati wa tafrija ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaa.

Bw. Daniel Manupa na mkewe wakila kiapo cha ndoa yao.

Bw. Nasson Mwandumbya na mkewe wakiwa na nyuso za furaha wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.