Tuesday, May 3, 2016

MAFUNZO YA UTAALAMU WA GESI NA MAFUTA KWA WATAALAMU WA BIMA YAFANYIKA MAKAO MAKUU

TIMU YA WATAALAMU WA MASUALA YA  BIMA KATIKA GESI NA MAFUTA KITOKA INDIA ILIWASII NCHINI KUTOA MAFUNZO KWA MAOFISA WA BIMA IKIWA NI MOJA KATI YA MPANGO KAZI WA SHIRIKA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYAKAZI.

 
Picha ya pamoja kati ya naofisa wa Bima na wataalam (Wakufunzi) kutoka India.


Bw. PrakashBhawani General Manager JB BODA Insurance Brokers PVT. Ltd ambaye alikuwa ni mmoja wa wataalamu waliokuja toa mafunzo ya Bima katika sekta ya Gesi na Mafuta.


Kaimu Mkurugenzi Ndugu Sam Kamanga akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi hao. Upande wa kushoto wa Bw. Kamanga ni Bw. N.B. Menon (Executive Director) JB BODA Insurance Brokers PVT. Ltd


Mkurugenzi mtendaji aliwaalika wageni wetu kwenye chakula cha mchana kabla hawajaelekea uwanja wa Ndege na kurudi kwao India. Wageni kutoka JB BODA Insurance Brokers -India walifurahishwa na mapokezi pamoja na ukarimu walioupata kutoka Shirika la Bima. 

Mafunzo haya ni mwendelezo wa mpango wa uongozi wa juu uliofanya katika juhudi za kuwaongezea uwezo wafanyakazi. Mpaka sasa mafunzo mbali mbali yamefanyika na wataalamu kutoka nje katika maeneo yafuatayo;

  1. Re-Insurance Accounting, 
  2. Risk Management in Oil and Gas Insurance
  3. Oil and Gas - Local content
  4. Oil and Gas Insurance -overview
Mafunzo yanayoandaliwa kwa sasa ni AGRO-INSURANCE. Bima ya Kilimo. Shirika linaazimia kuwajengea uwezo wafanyakazi wake kwenye eneo hilo kwa sababu uongozi unafikiria kuwa eneo hilo ndilo litakuwa na fursa kubwa kwa siku za usoni hasa ukuzingatia kuwa serikali imeisha anzisha Benki ya wakulima. Napenye Benki hapakosekani fursa ya biashara za Bima. Kwa wale watakaokuwa na hamu ya kupata utaalamu huo tunaomba wawasiliane na kaimu Mkurugenzi wa Bima za Mali na Ajali Bw. Lazaro Bangilana. Kumbukeni kuwa darasa linakuwa na wanafunzi 15 tu na nafasi zitatolewa kwa watu 15 wa kwanza na kutakuwa na nafasi 5 za stand-by.

TEAMWORK